1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa ya kuwaasili watoto yaibuka Uganda

Admin.WagnerD29 Mei 2015

Haya yanaibuka kufuatia nyaraka zilizovuja, data za mahakama na mahojiano waliyofanyiwa maafisa, wahanga na wazazi waliotaka kuwaasili watoto.

https://p.dw.com/p/1FZ75
Bildergalerie Immaterielles Kulturerbe UNESCO Bigwala Kürbistrompete
Picha: UNESCO/James Isabirye

Uganda imetajwa kugeuzwa kuwa eneo ambalo raia wa kigeni wanaweza kwenda na kupata watoto wanaotaka kuwaasili kuwa rahisi sana, huku wakisaidiwa na kampuni za mawakili kufanikisha hilo kupitia mianya katika sheria za nchi zinazohusu watoto.

Salma Mkalibala alizungumza na Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la kulinda watoto nchini Uganda, Martin Kiiza, na kumuuliza nini kinachoendelea kutokana na tatizo la kuwaasili watoto kinyume na utaratibu kuwa kubwa.

Kusikiliza mahojiano haya bonyeza alama ya spika hapo chini.

Mwandishi: Salma Mkalibala

Mhariri: Saumu Yusuf