1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karzai ailaumu Pakistan

4 Desemba 2011

Kabla ya mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan mjini Bonn, rais Hamid Karzai wa Afghanistan ameishutumu Pakistan kwa kukwamisha mazungumzo na Taliban.

https://p.dw.com/p/13ME4
Afghan President Hamid Karzai speaks during the opening of the "Loya Jirga" or grand council in Kabul. Afghan President Hamid Karzai called Wednesday on elders assembled for a national conference to help create a fair framework for relations with the U.S. and find a part to peace for the turbulent country. (Foto:Musadeq Sadeq/AP/dapd)
Rais wa Afghanistan, Hamid KarzaiPicha: dapd

Karzai ameliambia jarida la habari la Spiegel kuwa Pakistan , ambayo inasusia mkutano huo, imekataa kuunga mkono juhudi za majadiliano na Taliban.
Mkutano wa Bonn unataka kutafuta mwelekeo kwa Afghanistan baada ya kujitoa kwa majeshi ya NATO, lakini ususiaji wa Pakistan umeleta pigo kwa mwelekeo kama huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle pia amesikitishwa na uamuzi wa Pakistan, akisema kuwa nchi hiyo itafaidika zaidi kutokana na amani nchini Afghanistan kuliko nchi jirani nyingine yoyote. Wakati huo huo , mjini Bonn jana , maelfu ya watu waliandamana mitaani kuupinga mkutano huo pamoja na jukumu la Ujerumani nchini Afghanistan.