KARLSRUHE:Watuhumiwa watatu wa ugaidi wakamatwa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARLSRUHE:Watuhumiwa watatu wa ugaidi wakamatwa

Muongoza mashtaka wa Ujerumani bibi Monika Harms amesema kwamba watu watatu wanaotuhumiwa kuwa magaidi waliokamatwa jana katika jimbo la Northrhine Westfalia wana mahusiano na mtandao wa kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Watuhumiwa hao watatu wanaaminika kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi la Islamic Jihad lenye matawi yake nje na ndani ya Ujerumani na wote wamepewa mafunzo katika kambi ya kundi hilo iliyo nchini Pakistan mwaka 2006.

Watuhumiwa hao inadaiwa walitengeneza mapipa 12 ya kemikali yenye uzito wa kilo 550 na uwezo wa kufanya uharibifu mkubwa.

Watuhumiwa hao wawili raia wa Ujerumani na mmoja raia wa Uturuki walikuwa wakichunguzwa na polisi tangu Desemba mwaka jana walipogunduliwa kuwa waliichunguza kambi ya jeshi la Marekani ya Hanau iliyo katika mji wa Ramstein kilomita 120 kutoka Frankfurt.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com