1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karibu mwaka mpya wa 2010

Saumu Mwasimba31 Desemba 2009

Idhaa ya kiswahili ya Deutsche Welle tunawatakia wasikilizaji wetu wote duniani na pia wasomaji wa tovuti yetu heri na baraka za mwaka mpya wa 2010.

https://p.dw.com/p/LHuM
Heri ya mwaka mpya kutoka BonnPicha: AP

New Zealand ndio nchi ya kwanza hii leo kuoona mwaka mpya wa 2010.Katika mji wa Auckland wananchi wameukaribisha mwaka mpya kwa kurusha fash fash. Mji wa Sydney Australia pia umeshaukaribisha mwaka mpya wa 2010.

Takriban umati wa watu wapatao milioni moja na nusu wamesherehekea mwaka mpya ki aina yake ikiwemo kufyatua fataki angani katika mji huo.

Maeneo mbalimbali duniani kwa sasa yamekuwa yakijiandaa na sherehe za mkesha wa mwaka mpya.

Polisi wamewekwa katika tahadhari katika miji mingi duniani dhidi ya mashambulio ambayo yanaweza kutokea katika mkesha wa mwaka mpya, hususan kufuatia jaribio la kulipua ndege ya Marekani lililotokea siku ya Krismas.

Ulinzi umeimarishwa pia katika nchi za Afghanistan na Pakistan, huku Thailand ikipiga marukufu fataki baada ya ajali ya moto iliyosababisha vifo vya watu 65 wakati wa mkesha wa mwaka mpya katika klabu moja ya usiku mjini Bangkok.