1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KARBALA: Watu takirban 10 wauwawa

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBV3

Watu takriban 10 wameuwawa na madarzeni kadhaa kujeruhiwa kwenye machafuko kati ya vikosi vya usalama na watu waliokuwa wamejihami na bunduki mjini Karbala.

Maelfu ya watu wamekusanyika mjini humo kuadhimisha mojawapo ya siku takatifu za madhehebu ya Shia.

Duru za polisi zinasema kundi la mahujaji walikasirishwa na sheria kali za usalama zilizowekwa wakati wa maadhimisho hayo na mapigano yakapamba moto wakati vurugu zilipoanza.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa na waumini wameamriwa waondoke kutoka eneo hilo.

Wakati haya yakiarifiwa, mshambuliaji wa kujitoa mhanga maisha amejilipua na kuwaua watu wasiopungua 11 na kuwajeruhi wengine kadhaa katika msikiti mmoja mjini Fallujah.

Maafisa wa polisi wanasema mshambuliaji huyo alilipua ukanda wa baruti alipokuwa miongoni mwa waumini waliokuwa katika sala ya jioni.

Shambulio hilo lililenga shehe mkuu wa msikitu huo ambaye anaaminiwa alikuwa mpinzani mkubwa wa kundi la kigaidi la Al Qaeda.