1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mafunzo

Karandinga: Unaniua Taratibu

Grace Kabogo
1 Machi 2017

Maisha yameimarika kwa wakaazi wa Donge la Maji tangu kampuni ya kusafisha chuma ilivyofunguliwa mjini humo na kutoa fursa za ajira.

https://p.dw.com/p/2YQTG
DW Crime Fighters Serienmotiv „Killing Me Softly“

Aida Kabange, mama anayelea mtoto peke yake, hivi karibuni alihamia mjini humo na kuanza kazi kama katibu muhtasi wa kiwanda hicho. Lakini mambo yanakwenda ndivyo sivyo, baada ya mtoto wa kiume wa Aida kuumwa. Wakati huo huo, mfanyakazi wa kiwanda hicho anaanguka na kufa kutokana na ugonjwa wa Malaria, kama dokta alivyobainisha. Au kuna ukweli mwingine uliojificha nyuma ya kifo hichi? Wakati Aida anajaribu kutafuta chanzo cha ugonjwa wa mtoto wake, anagundua kitu kibaya katika kiwanda hicho. Je yuko tayari kuhatarisha kila kitu ili kufichua siri chafu kwenye kiwanda cha kusafishia chuma?