KARACHI: Mvua kubwa zimesababisha vifo | Habari za Ulimwengu | DW | 25.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KARACHI: Mvua kubwa zimesababisha vifo

Takriban watu 220 wameuwawa katika mji wa Karachi nchini Pakistan kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Mvua hizo pia zimesababisha ukosefu mkubwa wa umeme.

Raia wenye hasira wamefanya vurugu kwa kuchoma matairi na kuyarushia mawe magari yanayopita barabarani.

Mtu mmoja ameuwawa katika vurugu hizo.

Hali mbaya ya hewa imeikumba Pakistan na nchi jirani yake ya India.

Wafanyakazi wa kutoa misaada waling’ang’ana mwishoni mwa wiki kusambaza misaada ya chakula kwa takriban watu laki mbili walioathirika kutokana na mafuriko katika jimbo la Andhra Pradesh kusini mwa India.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com