Kansela Merkel(CDU/CSU) ndiye mshindi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.09.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Kansela Merkel(CDU/CSU) ndiye mshindi

Chama cha CDU cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeripotiwa kupata wingi wa kura katika uchaguzi uliokamilika muda mchache uliopita

default

Kansela Angela Merkel wa chama cha CDU/CSU

Ushindi huo utamuwezesha Bibi Merkel kuunda serikali na chama cha Kiliberali cha FDP.Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na kituo cha televisheni cha ZDF chama cha CDU/CSU kimepata asilimia 33.5 ya kura zote na FDP kimepata asilimia 14.5

Guido Westerwelle während einer Wahlkampfveranstaltung in Magdeburg

Kiongozi wa FDP Guido Westerwelle

Kwa pamoja kura za vyama hivyo viwili vimevipiku vyama vyengine vitatu vikubwa vilivyosalia.Kutokana na hali hiyo Bibi Merkel ataweza kuvunjilia mbali muungano wa CDU na SPD uliokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mine iliyopita.Ushirikiano wao na chama cha Kiliberali cha FDP kinachounga mkono masuala ya biashara utamuwezesha Bibi Merkel kuyapa msukumo zaidi masuala ya kupunguza kodi pamoja na kuuongeza muda wa kuvitumia viwanda vya nuklia.Chama cha Kisoshalisti cha SPD kimeripotiwa kupata asilimia 23.5 takwimu zinazoaminika kuwa za chini zaidi tangu kukamilika kwa vita vikuu vya dunia.Chama cha Kijani Grüne kimepata asilimia 10 nacho cha mrengo wa shoto Die Linke nacho kimejikusanyia asilimia 13.

Bibi Merkel anapendwa

Tofauti na hali ilivyokuwa Marekani na Japan wapigaji kura wa Ujerumani hawakuonekana kutaka mabadiliko ya uongozi uliokuwapo.Wengi wnaaripotiwa kuwa na imani na mfumo wa Bibi Merkel ambaye ni Kansela wa kwanza wa kike wa Ujerumani na ni mgombea pekee wa ngazi hiyo anayetokea eneo la Mashariki lililokuwa likisimamiwa na utawala wa Kikomunisti.

Uchaguzi huu unafanyika wakati muhimu ambapo Ujerumani iliyo na uchumi wa tatu kwa ukubwa barani Ulaya inajikwamua kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliougubika ulimwengu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Serikali mpya italazimika kupambana na bajeti inayokabiliwa na madeni,uhaba mkubwa wa kazi pamoja na athari zilizosababishwa na mparaganyiko wa kiuchumi jambo ambalo litayafanya mabenki kuvipunguza viwango vyao mikopo inayotoa.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya-RTRE/DPAE

Mhariri:Othman Miraji

DW inapendekeza

 • Tarehe 27.09.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Jq90
 • Tarehe 27.09.2009
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Jq90

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com