1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel kukutana na Waziri Mkuu Olmert mjini Jerusalem

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOxu

BERLIN:

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kabla ya kuanza ziara yake siku ya Jumapili nchini Israel amesema,azma ya ziara hiyo hasa ni kuendeleza uhusiano wa pande mbili.Katika ujumbe wake wa kila juma kwenye mtandao wa Intaneti Merkel amesema,yeye na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert wamekubaliana kuwa katika siku zijazo,serikali za nchi hizo mbili zikutane kwa majadiliano kila mwaka.

Majadiliano ya kwanza yatakuwa siku ya Jumatatu mjini Jerusalem.Kansela Merkel anafuatana na ujumbe mkubwa na miongoni mwa wajumbe hao ni mawaziri wake saba.Sababu ya ziara hiyo ni kutimiza kwa miaka 60 tangu kuundwa taifa la Israel.Wabunge wa Ujerumani wanaohusika na sera za nje wamemuomba Merkel wakati wa ziara hiyo nchini Israel azungumzie pia suala nyeti linalohusika ujenzi wa makaazi ya Wayahudi.