1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Merkel azungumza na maripota

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Kansela Merkel atetea uamuzi wa kuwepo wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan

https://p.dw.com/p/G6CO


Berlin:

Kansela Angela Merkel anapanga kutetea katika kampeni zijazo za uchaguzi, uamuzi wa kutumwa wanajeshi wa Bundeswehr nchini Afghanistan.Katika mahojiano pamoja na gazeti la FRANKFURTER ALGEMMEINE SONNTAGSZEITUNG,mwenyekiti huyo wa chama cha CDU,amepinga madai ya kuwarejesha nyumbani wanajeshi hao.Kansela Angela Merkel amesema wanajeshi wa Bubndeswehr watarejea nyumbani ikiwa Afghanistan itakua katika hali ya kuweza kujihami,na kama itakua na serikali imara..Hata hiovyo kansela Angela merkel ameondowa uwezekano wa kuzidishwa idadi ya wanajeshi hao nchini Afghanistan.