1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansa huathiri watoto walio karibu na mitambo ya nuklea

8 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZAi

BERLIN

Utafiti wa serikali ya Ujerumani umegunduwa kwamba watoto wanaoishi karibu na mitambo ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea wako rahisi zaidi kupata ugonjwa wa kansa ya damu au wa kansa ya mifupa.

Ujerumani hivi sasa ina mitambo 16 ya kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea ambayo yote inatazamiwa kufungwa ifikapo mwaka 2022.Utafiti huo uliofanywa na Mrajisi wa Kansa ya Watoto nchini Ujerumani umesema kwamba watoto 37 wanaoishi umbali usiozidi kilomita 5 kutoka mitambo hiyo wamekuja kuathirika na kansa ya damu katika kipindi kati ya mwaka 1980 na mwaka 2003.

Wastani wa takwimu nchini Ujerumani ungeliweza kutabiri kesi 17 katika kundi hilo la watoto.

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema kamati ya serikali ya viwango vya usalama vya sumu ya miale ya nuklea itachanganuwa utafti huo.