1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanda ya euro kuidhinisha mkopo wa Ugiriki

20 Februari 2012

Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya euro leo hii wanatarajiwa kupitisha awamu ya pili ya mkopo wa kiasi cha euro bilioni 130 kwa lengo la kuinusuru Ugiriki isifilisike.

https://p.dw.com/p/145qT
epa03099349 Protesters shout slogans and wave red flags during a general strike protest in Athens, Greece, 10 February 2012. Greek trade unions called for a 48-hour general strike to oppose new austerity measures. EPA/ORESTIS PANAGIOTOU +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waandamanaji AthensPicha: picture-alliance/dpa

Mkutano huo wa leo, utaonesha muelekeo wa jitihada za nchi za kanda ya euro baada ya misukosuko ya kuioka Ugiriki iliyodumu kwa miezi kadhaa na ambayo pia pamoja na athari nyingine imeiyumbisha sarafu yake. Ingawa bado kuna kazi kubwa katika kufanikisha upatikanaji wa tija ya mkopo huo.

Wanadiplomasia na wachumi hawatarajii kitita hicho cha fedha kwa Ugiriki kitatatua tatizo sugu la kiuchumu la taifa hilo, kwa kusema itachukua muongo mmoja au zaidi kuondoshwa taswira ya ongezeko la maandamano ya maelfu ya raia wa nchi hiyo ambao jana waliingia mitaani kupinga hatua kali ya serikali yao kubana matumizi.

Hata hivyo mawaziri hawa wa fedha wa kanda ya euro bado wanataka kukubaliana hatua mpya zaidi kuweka sawa mambo kabla ya kutoa kiasi hicho cha fedha kwa taifa hilo lililoporomoka vibaya kiuchumi.

French Finance Minister Francois Baroin, right, and Luxembourg's Prime Minister Jean-Claude Juncker, left, speak with German Finance Minister Wolfgang Schaeuble during a meeting of eurozone finance ministers at the EU Council building in Brussels on Monday, Nov. 7, 2011. Greece's two biggest parties resumed talks Monday to agree on who should be the country's new prime minister, after reaching a historic power-sharing deal to accept a massive financial rescue package and prevent imminent bankruptcy. Fellow European governments will want concrete progress by the evening, when eurozone finance ministers meet to discuss the possibility of unfreezing bailout loans that had been kept on hold while the country sorted its political turmoil. (AP Photo/Virginia Mayo)
Mawaziri wa fedha wa EUPicha: AP

Lakini kuna matumaini kwamba makubaliano haya yatasaidia kuinusuru Ugiriki na hali mbaya ya kuichumi, kuiweka imara kiuchumi na kuifanya iendelee kuwepo katika nchi zinazotumia sarafu ya euro.

Hapo jana maafisa waandamizi kutoka wizara za fedha za nchi zinazotumia sarafu ya euro pamoja na Benki ya Kuu ya Ulaya walikutana kupitia taarifa ya mwisho ya mpango wa euro bilioni 130 ikijumuisha, pamoja na uchambuzi wa kuhimili madeni kwa Shirika la Fedha Duniani, IMF.

Haya yanatarajiwa kufanyika huku kukiwa na shaka kwa Ujerumani na mataifa mengine kama Ugiriki kutimiza ahadi zake kufanikisha upatikanaji wa kiasi cha euro bilioni 3.3 katika makato mbalimbali pamoja na kuongeza tozo la kodi.

Pamoja na wasiwasi huo, Waziri wa Fedha wa Ufaransa, Francois Baroin, na wa Austria, Maria Fekter, wamesema wana kila kitu kitakachosababisha wapitishe mkopo huo wa uokozi.

Katika mkutano wa jana wa maafisa waandamizi wa kanda hiyo uliojumisha pia mawaziri wadogo wa fedha, kulielezwa kwamba kuna masuala madago madogo ambayo yalipaswa kurekebishwa. Ingawa pia walisema masuala hayo hayawezi kukwamishwa mchakato mzima.

Huko Ugiriki kwenyewe kumegubigwa na maandamano ambapo jana idadi kubwa ya watu waliingia barabarani kupinga vikali hatua za kubana matumizi za serikali ya nchi hiyo.

Hata hivyo waziri wa Mkuu wa taifa hilo, Lucas Papademos, jana aliripotiwa kuondoka nchini humo kuelekea mjini Brussels nchini Ubelgiji kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa leo.

Mwandishi: Sudi Mnette//RTR

Mhariri:Josephat Charo