1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA.Uganda kuweka kamera za kuchunguza nyendo za watu kabla ya mkutano wa jumuiya ya madola

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBas

Uganda itakuwa nchi ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki kuwa na camera za kisasa za kuchunguza mienendo ya watu kwenye barabara za miji.

Kamera hizo zitakazoanza kuwekwa mwezi huu zinanuiwa kuimarisha hali ya usalama katika nchi hiyo kabla ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya madola mnamo mwezi Novemba.

Kamera 24 zitawekwa katika mji mkuu Kampala na nyingine tatu zitaweka katika eneo la karibu na Ziwa Victoria ambako malkia Elizabeth wa Uingereza na viongozi wengine watakutana.

Kamera hizo za kunasa matukio katika barabara za miji zitakuwa zikichunguzwa na polisi katika kituo maalum katika ubalozi wa zamani wa uingereza mjini Kampala.

Maandalizi ya mkutano huo yanaendelea nchini Uganda ambapo wajenzi wanajitahidi kumaliza kujenga hoteli zitakazoweza kukimu malazi ya wageni watakaohudhuria mkutano huo.