1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Mamilioni wahitaji msaada babada ya kukumbwa na mafuriko

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOi

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetoa wito wa kupatiwa msaada wa zaidi ya dola millioni 65 kwa ajili ya wahanga wapatao milioni 1 na laki saba wa mafuriko makubwa yaliyoyakumba maeneo kadhaa ya afrika.

Huko Kaskazini mwa Uganda imearifiwa kuwa watu tisa wameuawa na wengine zaidi ya laki moja unusu hawana makazi kutokana na mafuriko hayo.

Michael Nataka ni kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Uganda.

Nchini Somalia Waziri wa mambo ya ndani Mahamoud Guled amewaambia waandishi wa habari ya kwamba eneo la kusini mwa nchi hiyo linakabiliwa na janga kubwa la kibinaadamu.

Hali hiyo inatokana na mafuriko makubwa kulikumba eneo hilo ambapo mashamba , mifugo na nyumba vimesombwa na maji.