1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA: Wakimbizi watahamishwa usalama ukiimarika

Umoja wa Mataifa umeahirisha kuhamisha wakimbizi kutoka kambi za kaskazini ya Uganda na kupelekwa kusini mwa Sudan.Uamuzi huo umepitishwa baada ya hadi watu 40 kuuawa na watu wenye silaha wasiojulikana kusini mwa Sudan,siku ya Jumatano na Alkhamisi.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi limesema wakimbizi hawatohamishwa mpaka hali ya usalama itakapokuwa bora.Inadhaniwa kuwa mashambulio hayo yanahusika na mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na kundi la waasi la LRA.Hivi sasa kambini nchini Uganda na nchi zingine za jirani kuna wakimbizi 350,000 kutoka kusini mwa Sudan.Wengine milioni 4 wamepoteza maskani zao nchini Sudan kwa sababu ya vita vya miaka 21.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com