1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Polisi yavunja maandamano ya upinzani

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCra

Vikosi vya usalama vya Uganda leo vimefyatuwa mabomu ya kutowa machozi na kurusha maji ya pili pili kuwatanwanya mamia ya wafuasi wa upinzani katika maandamano yaliopigwa marufuku kwenye mji mkuu wa Uganda Kampala.

Polisi pia iliendesha mapambano ya kufukuzana mitaani na baadhi ya wapizani wanaofikia 800 waliokaidi amri ya kupiga marufuku wito wa kujitokeza kwenye Uwanja wa Katiba kumuunga mkono kongozi wa chama cha upinzani cha FDC Kizza Besigye.

Hakuna repeoti zilizopatilkana mara moja juu ya majeruhi kutokana na vurugu hizo zilizozuka wakati polisi ilipojaribu kuuzuwiya msafara wa magari ya Besigye kuingia uwanjani hapo kuzinduwa kampeni ya kuandikisha wanachama ambayo serikali imesema sio halali.