1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamishna ataka jeshi la Ujerumani liongezwe

27 Desemba 2015

Kamishna wa bunge anayeshughulikia jeshi la Ujerumani ametowa wito wa kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi hao kukabiliana na migogoro duniani ambapo amesema angalau kikosi hicho kiongezewe wanajeshi 7,000.

https://p.dw.com/p/1HUD6
Wanajeshi wa Ujerumani.
Wanajeshi wa Ujerumani.Picha: Reuters/F. Bimmer

Kamishna wa bunge anayeshughulikia jeshi la Ujerumani ametowa wito wa kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi hao kukabiliana na migogoro duniani ambapo amesema angalau kikosi hicho kiongezewe wanajeshi 7,000.

Hans- Peter Bartels amesema katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba "wanajeshi katika jeshi la Ujerumani la Bundeswehr wamekuwa wakipunguwa moja kwa moja kwa miaka 25."

Ujerumani ilikuwa na takriban wanajeshi 600,000 mara tu baada ya kuungana tena kwa iliokuwa Ujerumani ya mashariki na magharibi lakini hivi sasa jeshi hilo limebakiza wanajeshi 178.000 tu.

Amesisitiza kwamba "Jambo hilo lazima libadilike tena. Haiwezekekani kwa jeshi hilo kuendelea kupunguwa lazima liongezeke."

Haja ya kuongezwa idadi ya wanajeshi

Kwa muijibu wa takwimu za kamishna huyo jeshi hilo inabidi liongezeke tena kufikia wanajeshi 185,000 kama ilivyotakiwa na mageuzi ya jeshi la Ujerumani Bundeswehr ya mwaka 2010.Ameuliza kwanini wasifikie wanajeshi 187,000 au hata zaidi ? Kwani inabidi ifikiwe idadi inayotakiwa hasa kwa mujibu wa miundo ambayo imepangwa.

Kamishna wa bunge anayeshughulikia jeshi la Ujerumani Hans-Peter Bartels.
Kamishna wa bunge anayeshughulikia jeshi la Ujerumani Hans-Peter Bartels.Picha: picture-alliance/dpa/S. Stache

Wizara ya ulinzi hivi sasa inaangalia namna ya kuimarisha uwezo wa jeshi hilo ambapo matokeo yake yanatarajiwa kutolewa katika kipindi cha majira machipuko.

Kwa mujibu wa Bartels katika matawi mengi ya jeshi hilo uwezo wao umekuwa na kikomo. Kamishna huyo anatowa wito miongoni mwa mambo mengine kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi wa kujitolea kuhudumia taifa katika shughuli nzito.Kwa sasa kuna kazi 5,000 tu za aina hiyo juu ya kwamba kwa wastani wanajeshi wa kujitolea 10,000 wako kazini.

Nafasi za kazi nzito zinatakiwa ziwe za uhakika na majukumu yake yakiainishwa wazi wazi. Kwa ajili ya kupata nafasi hizo kwa wajiriwa wa kujitolea kunakuwa hakuna njia ya wazi ya kuwajumuisha kwenye miundo ya jeshi la Ujerumani Bundeswher.

Ongezeko kwa bajeti pia

Kamishna huyo pia anapendelea kuongezwa kwa kima kikubwa bajeti ya ulinzi.Amesema ongezeko la bajeti la euro bilioni 35 kutoka bilioni 33 kufikia mwaka 2019 halitoshi.Sehemu ambayo matumizi hayo ya kijeshi inachukuwa kutoka pato la jumla la taifa itashuka kutoka asilimia 1.16 na kuwa asilimia 1.07 hapo mwaka 2019.

Wanajeshi wa Ujerumani.
Wanajeshi wa Ujerumani.Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Kwa upande mwengine waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble anataraji matumizi kwa ajili ya opesheni za kijeshi katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya yataongezeka kutokana na mzozo wa wakimbizi kwa hiyo ametaka kuundwe jeshi la Umoja wa Ulaya.

Ameliambia gazeti la "Bild am Sonntag" kwamba inabidi watumie fedha zaidi kwa harakati za ulinzi za pamoja za Umoja wa Ulaya na kwamba sera za kigeni na ulinzi za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya lazima ziunganishwe hatua kwa hatua.

Jeshi la Ulaya

Amesema hatimae lengo linapaswa kuwa na jeshi moja la Ulaya ambapo fedha zinazotumiwa na majeshi ya mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaweza kutumiwa kwa pamoja kwa ufanisi zaidi.

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble.
Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble.Picha: picture-alliance/dpa/J. Warnand

Mwanasiasa huyo wa chama cha CDU anaona mzozo wa wakimbizi umepelekea Umoja wa Ulaya kujihusisha kwa pamoja kwa nguvu zaidi katika maeneo ya mizozo duniani ambapo kwa Ujerumani hiyo inamaanisha ushiriki wao unahitajika zaidi katika sera ya kigeni na ulinzi ya umoja wa Ulaya.

Schäuble aonaona hakuwezi kuwepo utengamano Mashariki ya Kati wala Afrika bila ya Ulaya kujitolea kwa nguvu kukabiliana na mizozo ya maeneo hayo.

Mwandishi : Mohamed Dahman/dpa(dw

Mhariri : Amina Abubakar