1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak apendekeza kupunguza idadi ya wanajeshi

Josephat Charo11 Septemba 2007

Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak, David Patraeus, amesema kuna ufanisi uliopatikana katika harakati ya kijeshi nchini Irak.

https://p.dw.com/p/CB1O
Jenerali David Patraeus (kushoto) na rais George W Bush wa Marekani
Jenerali David Patraeus (kushoto) na rais George W Bush wa MarekaniPicha: AP

Kamanda mkuu wa jeshi la Marekani nchini Irak, jenerali David Patraeus, amependekeza wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak wapunguzwe kufikia msimu ujao wa kiangazi.

Wanajeshi 30,000 wa Marekani huenda wakaondolewa kutoka Irak kufikia katikati ya mwaka ujao 2008 na wanajeshi 2,000 huenda wakaanza kuondoka katika majuma machache yajayo.

Akiwasilisha ripoti yake katika bunge la Marekani, jenerali Petraeus, amesema malengo ya kijeshi kwa kiwango kikubwa yanafanikiwa na kwamba wanajeshi wa Marekani na wa Irak wamepata ufanisi mkubwa katika kudumisha usalama licha ya kukabiliwa na maadui hatari na joto kali la msimu wa kiaganzi nchini Irak.

Hata hivyo jenerali Petraeus ameonya kwamba hali bado ni ngumu nchini Irak na muda unahitajika kujatimiza malengo yanayonuiwa.

´Tukizingatia hali nchini Irak bado ni ngumu na mara nyingine ya kuvunja moyo. Pia ninaamini inawezekana kuyatimiza malengo yetu katika kipindi fulani ingawa kufanya hivyo hakutakuwa haraka wala rahisi.´