1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kalou: Nataka kushinda mataji Hertha Berlin

29 Januari 2016

Mshambuliaji wa Hertha Berlin Salomon Kalou ana magoli tisa aliyofunga katika Bundesliga msimu huu. Lakini ana hamu ya kuleta mataji katika klabu hiyo ya mji mkuu wa Ujerumani, kama alivyofanya akiwa England

https://p.dw.com/p/1Hlz1
Bundesliga Hannover 96 - Hertha BSC
Picha: picture-alliance/dpa/P. Steffen

Katika mahojiano na DW, Kalou anasema ameanza saa kuyaozea maisha ya Bundesliga. "Niliwasili mwaka jana. ilikuwa mara yangu ya kwanza katika Bundesliga na pia nilikuwa nacheza katika timu mpya na wachezaji wapya. nadhani mwaka huu nimepata muda wa kushirikishwa zaidi katika timu. nilikwenda kwenye kambi za mazoezi ya timu. Nimezoeana na wachezaji wenzangu. na nadhani hilo pia limenisaidia kufanya vyema msimu huu".

Hertha Berlin inashikilia nafasi ya tatu kwa sasa katika msimamo wa Bundesliga, na kikosi kinajitahidi kuhakikisha kuwa kinacheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Kalou aliwahi kushinda taji la Champions League akiwa na Chelsea, na anasema kwa sasa ana motisha kubwa kujaribu kufanya vyema katika jukwaa hilo la Ulaya "nadhani Champions League ni kinyang'anyiro cha kusisimua sana barani Ualya. na kucheza kucheza katika Champions League ni kama jukwaa la kila mchezaji kuonyesha ujuzi wake, kujilinganisha na wachezaji wengine. Hivyo nadhani msimu huu kwa klabu ya Hertha Berlin, ni fursa nzuri ya kujaribu kukuza kandanda letu na namna tunavyocheza. na pia mashabiki wetu, wanataka kutuona tukicheza dhidi ya vilabu vikubwa. Hivyo nadhani kila mmoja ana motisha kutimiza lengo hilo pamoja. lakini nadhani hatupaswi kujiwekea shinikizo. nadhani tukicheza vyema michuano 17 iliyosalia msimu huu katika Bundesliga, tunaweza kufuzu katika dimba la Kombe la Mabingwa Ulaya msimu ujao".

Ni Salomon Kalou mchezaji wa timu ya taifa ya Cote d'Ivoire ambaye anachezea klabu ya Hertah Berlin hapa Ujerumani katika mahojiano na DW.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Daniel Gakuba