1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.Watu 41 wauwawa katika wimbi la mashambulizi ya mabomu.

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVu

Wimbi la mashambulizi ya mabomu na mapigano yaliyoripotiwa nchini Afghanistan jana Jumamosi yamesababisha vifo vya watu 41 na wengine sita kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na raia wawili wa kigeni ambao wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga karibu na mji mkuu.

Ghasi zinazofanywa na wapiganaji zimeongezeka kwa kiwango cha juu kabisa hivi sasa tangu pale majeshi ya Marekani kuivamia nchi hiyo mwaka 2001 katika azma ya kuwaondoa watawala wenye imani kali ya kidini wa Taliban , ambao walikuwa wakishirikiana na kundi la kigaidi la al-Qaida kufuatia shambulio la Septemba 11 nchini Marekani.

Ghasia nyingi zinatokea katika maeneo ya kusini na mashariki ya Afghanistan, maeneo ambayo wapiganaji wamekuwa wakifanya mashambulizi kadha siku ya Jumamosi, lakini kumekuwa pia na matukio kadha ya mabomu ya kujitoa muhanga dhidi ya majeshi ya ulinzi ya nchi hiyo pamoja na yale ya kigeni.

Wakati huo huo uchunguzi unafanyika kutokana na vifo vya wanajeshi watatu wa Uingereza katika shambulio la bomu lililodondoshwa na ndege ya kijeshi ya Marekani ambalo lilikuwa limelengwa kwa waasi wa Taliban.

Tukio hilo lililotokea upande wa jimbo la kusini la Helmand siku ya Alhamis lilikuwa baya kabisa katika wimbi la matukio kama hayo ya kimakosa katika kampeni ya kimataifa inayoongezeka dhidi ya wapiganaji wa Taliban wanaoungwa mkono na al-