1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Watakeji waongeza muda kwa mateka wao wa kifaransa

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4X

Wanamgambo wa kitalaban nchini Afghanistan wamerefusha muda wa mwisho kwa mateka wa kifaransa wanamshikilia hadi kukamilika kwa uchaguzi wa nchi hiyo hii leo.

Hicho ni kipindi cha pili cha ziada kurefushwa na wanamgambo hao, ambao waliwakamata wafaransa wawili waliyokuwa wakifanyakazi katika shirika la misaada kwa watoto kusini mwa Afghanistan.Mmoja tayari amekwishaachiwa.

Wakati huo huo polisi wanane wa Afghanistan wameuawa kufuatia kushambiliwa na wapiganaji wa kitaliban katika jimbo la Magharibi la Farah.