1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Wapiganaji 100 wakitaliban wauwawa

29 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUy

Wanajeshi wanaongozwa na Marekani pamoja na wale wa Afghanstan wamewauwa zaidi ya wapiganaji 100 wakitaliban katika mapambano yaliyozuka kusini mwa Afghanstan.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo la muungano nchini Afghanstan imesema mwanajeshi mmoja wa Afghanstan aliuwawa na watatu wa kikosi cha muungano walijeruhiwa kwenye mapigano.

Mapamabano hayo yalitokea baada ya wanajeshi wanaoongozwa na Marekani kuvamiwa na kundi kubwa la wapiganaji wakitaliban.

Ndege za kijeshi ziliharibu maskani za wapiganaji.