1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL:Sita wahojiwa juu ya mauaji ya wandishi habari wa Deutsche Welle nchini Afghanistan

Maafisa wa idara ya usalama nchini Afghanistan wanawahoji watu sita juu ya mauaji ya waandishi habari wawili wa kijerumani nchini humo. Wandishi hao waliokuwa wanafanya kazi kwa niaba ya Deutsche Welle waliuliwa kwa kupigwa risasi ndani ya hema lao katika jimbo la Baghlan umbali wa kilometa 120 kaskazini ya mji mkuu Kabul.

Kabla ya kuuawa waandishi hao waliokuwa wanafanya utafiti, walikuwa pamoja na askari wa Ujerumani ambao ni sehemu ya jeshi la NATO linalolinda amani nchini Afghanistan.

Lakini walikuwa njiani peke yao kuelekea katika mji mwingine.

Tuhuma juu ya wandishi hao kuuliwa na wapiganaji wa kitaliban zimekanushwa na msemaji wa wapiganaji hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com