1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Shambulizi lingine la kujitoa mhanga latokea Afghanistan

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz1

Mshambulaji wa kujitoa mhanga amejilipua na kuuwa watu wawili huku wengi wanne wakijeruhiwa, katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

Mshambuliaji huyo, ambaye alikuwa akiendesha pikipiki, alijilipua karibu na askari waliyokuwa wakifanya doria katika barabara kuu ya Jalalabad.

Wapiganaji wa Taleban wamedai kuhusika na shambulizi hilo.Katika hatua nyingine Askari mmoja wa Finland aliyeko kwenye kikosi cha NATO, ameuawa pamoja na raia mmoja kutokana na shambulizi la bomu huko kaskazini magharibi mwa Afghanistan.

Kumekuwa na ongezeko kubwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga na mabomu, nchini humo katika siku za hivi karibuni.