1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Watu wanane wanahojiwa kwa mauaji

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKi

.

Watu wanane wamekamatwa baada ya mfanyakazi wa kutoa misaada raia wa Ujerumani kupigwa risasi na kufa kaskazini ya Afghanistan , gavana wa eneo hilo amesema jana Ijumaa , na kuongeza kuwa haifahamiki iwapo wauaji hao ni wapiganaji wa Kiislamu ama ni majambazi tu.

Mjini Berlin , shirika la misaada ya chakula la Ujerumani Deutsche Welthungerhilfe, limesema linaamini kuwa mhandisi huyo mwenye umri wa miaka 65 aliuwawa kutokana na masuala ya kisiasa.

Polisi wanawahoji watu hao wanane, ambao walikamatwa katika jimbo la Faryab, ambalo ni jirani na jimbo la Sari Pul , ambako mtu huyo alipigwa risasi siku ya Alhamis, amesema gavana wa jimbo la Sari Pul Iqbal Munib.Watu wenye silaha walipora mali za Waafghanistan watatu ambao walikuwa wakisafiri na Mjerumani huyo kabla ya kuwaachia.