1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Watu waanza maombolezo baada ya shambulio la kujitoa muhanga kuuwa watu 40.

7 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79A

Nchini Afghanistan watu wameanza siku tatu za maombolezi, kufuatia shambulio la kujitoa muhanga kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu kiasi 40 wameuwawa na wengine 100 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo, ambalo limesababisha wabunge sita kuuwawa , lilitokea wakati ujumbe wa ngazi ya juu ulipotembelea kiwanda cha sukari katika jimbo la Baghlan.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amesisitiza haja ya kuimarisha ulinzi ili kuleta amani katika nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-walter Steinmeier ameshutumu shambulio hilo , akilieleza kuwa ni jaribio la kuzuwia ujenzi mpya nchini humo. Steinmeier amesema katika taarifa kuwa kiwanda hicho cha sukari ni moja kati ya miradi iliyokuwa inalindwa na jeshi la Ujerumani lililoko nchini humo kama sehemu ya jeshi la kimataifa la kusaidia kuleta usalama linaloongozwa na NATO.