1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Watu 60 wafa maji Afghanistan

Watu kiasi sitini, wakiwemo watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Taliban, wamekufa maji walipojaribu kuvuka mto kusini mwa Afghanistan.

Wizara ya Ulinzi imesema mashua iliyowabeba watu hao ilipinduka jana katika mto wa Helmand.

Wizara hiyo inafanya uchunguzi ili ibainishe idadi ya raia na pia idadi ya wanamgambo walioangamia.

Mapema mwezi Machi, majeshi ya Afghanistan yakishiriana na vikosi vya NATO, yalianzisha harakati za kijeshi katika mkoa wa Helmand ambao ndio ngome kuu ya wanamgambo wa Taliban.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com