KABUL: Wataliban wakubali kukutana na wajumbe wa Korea | Habari za Ulimwengu | DW | 03.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Wataliban wakubali kukutana na wajumbe wa Korea

Maafisa nchini Afghanistan wamesema,wanamgambo wa Taliban wanaowazuia mateka raia 21 wa Korea ya Kusini,sasa wapo tayari kufanya mazungumzo ya ana kwa ana pamoja na maafisa wa Korea.Wateka nyara hao wameshawaua Wakorea 2 kutoka jumla ya 23 waliotekwa nyara.Wanamgambo wa Taliban wanaitaka serikali ya Afghanistan iwatoe jela wafungwa wa Taliban na badala yake mateka wa Korea ya Kusini wataachiliwa huru.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com