1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wafanyakazi wa Deutsche Welle wameuawa Afghanistan

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4s

Waandishi wa habari 2 wa kujitegemea wa Deutsche Welle wameuawa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa Afghanistan.Karen Fischer aliekuwa na umri wa miaka 30 na Christian Struwe wa miaka 38 waligunduliwa ndani ya hema,Jumamosi asubuhi katika wilaya ya Baghlan,kama kilomita 120 kaskazini ya mji mkuu wa Afghanistan,Kabul. Waandishi wa habari hao walilifahamu vizuri eneo hilo na walikuwa wakitayarisha kipindi cha kuonyesha hali halisi na walikuwa wakifanya uchuguzi wao wenyewe na si kwa niaba ya Deutsche Welle.Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle,Erik Bettermann ametoa rambi rambi kwa familia za waandishi wa habari hao 2 na amesifu mchango wao katika shughuli za kujenga upya mfumo wa vyombo vya habari nchini Afghanistan.Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amelaani vikali mauaji hayo na anataka uchunguzi ufanywe na hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika.