1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Taliban wawakamata raia wa Ufaransa.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCR

Wapiganaji wa Taliban wamewakamata raia wawili wa Ufaransa katika jimbo la magharibi la Afghanistan la Nimroz. Msemaji wa kundi hilo amesema kuwa raia watatu wa Afghanistan waliokuwa pamoja na Wafaransa hao pia wamekamatwa na kundi hilo la Taliban. Hapo mapema wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa na wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan zilithibitisha kuwa watu hao watano ambao ni wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada wanaofanyakazi katika shirika la kutoa misaada la Ufaransa la Terre d’Enfance wamepotea tangu siku ya Jumanne.