1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Operesheni za kijeshi zaendelea Afghanistan

7 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBl4

Zaidi ya wanamgambo 100 wa Taliban wameuawa nchini Afghanistan katika mapigano yaliyozuka tangu siku ya Ijumaa,kati ya vikosi vya serikali na majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani. Hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa majeshi hayo. Wakati huo huo wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan,mjini Kabul imesema,inachunguza ripoti ya wakazi wa vijijini kwamba kwa mara nyingine tena,raia wameuawa katika operesheni za majeshi.