1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Mwandishi aachiwa huru.

Mwandishi habari raia wa Italia ambaye alikuwa akishikiliwa mateka kwa muda wa wiki mbili na wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan ameachiliwa huru.

Waziri mkuu wa Italia Romano Prodi amethibitisha kuwa Daniele Mastrogiacomo alikuwa katika hali nzuri na alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali inayoendeshwa na Wataliani katika jimbo la Helmand.

Mastrogiacomo alikamatwa karibu na eneo hilo mapema mwezi huu wakati alipokuwa akisafiri kwenda kukutana na kamanda wa Taliban.

Wapiganaji hao walitishia kumuua Mastrogiacomo hadi pale viongozi watatu wa Taliban walioko jela watakapoachiliwa na serikali ya Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com