1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Mkutano wa madawa ya kulevywa wafunguliwa.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B1

Mkutano wa kimataifa kuhusiana na madawa ya kulevywa umefunguliwa nchini Afghanistan kwa wito wa ushirikiano wa kimkoa katika vita dhidi ya uzalishaji na usafirishaji wa bangi katika eneo la kati la bara la Asia. Wataalamu kutoka serikalini kutoka mataifa 55 wanakutana mjini Kabul kwa mkutano wa siku mbili.

Mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevywa wa umoja wa mataifa Antonio Maria Costa amesema kuwa mavuno ya madawa ya kulevywa nchini Afghanistan yanaleta kitisho kikubwa kwa afya ya jamii duniani kote na pia kwa usalama wa mataifa jirani ya Asia ya kati. Kwa mujibu wa umoja wa mataifa Afghanistan ni karibu mzalishaji mkuu wa madawa hayo . Uzalishaji wa madawa ya kulevywa nchini Afghanistan umepanda kwa zaidi ya theluthi moja na kufikia kiwango cha juu mwaka 2007 na ikiwa faida ya asilimia 90 ikienda kwenye makundi ya uhalifu na umtandao wa kigaidi.