1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Merkel arejea kutoka ziarani Afghanistan.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A5

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa anatarajia majeshi ya Ujerumani yaliyoko nchini Afghanistan yataendelea kutumikia kwa muda mrefu nchini humo.

Alikuwa akizungumza baada ya kurejea kutoka katika ziara yake ya kwanza nchini humo jana Jumamosi.

Ujerumani hivi sasa ina wanajeshi wapatao 3,000 wanaotumika nchini Afghanistan, hususan upande wa kaskazini ambao hali ni shwari.

Wakati wa ziara yake kansela Merkel ameondoa uwezekano wa majeshi ya Ujerumani kuwekwa katika maeneo ya hatari zaidi upande wa kusini mwa nchi hiyo.