1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Merkel aahidi kusaidia polisi wa Afghanistan

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AE

Kansela Angela yuko kwenye ziara ambayo haikutangazwa nchini Afghanistan kwa sababu za kiusalama.

Katika ziara yake hiyo ya kwanza rasmi nchini Afghanistan ameahidi kwamba serikali ya Ujerumani itaongeza juhudi zake za kuimarisha kikosi cha polisi cha nchi hiyo ambacho kinaonekana kuwa ni muhimu katika kujaribu kuzima tishio la mauaji ya kuijitolea muhanga maisha na mabomu yanayotegwa pembezoni mwa barabara.

Merkel akizungumza baada ya kukutana na Rais Hamid Karzai amesema ataangalia kuona iwapo serikali yake inaweza kutenga fedha zaidi kwa kazi hiyo katika bajeti yake ya mwaka 2008.

Merkel anasema mafunzo ya polisi hao ni kipengee kikuu ili kwamba wananchi wa Aghanistan waweze kuishi maisha halisi katika nchi yao kadhalika katika kusghulikia mashaka yao ya usalama.

Kama taifa linaloongoza kutowa mafunzo kwa polisi wa Afghanistan Ujerumani imetumia euro milioni 74 kwa kikosi hicho tokea mwaka 2002.

Baada ya kukutana na Karzai na viongozi wa kijeshi pamoja na wanadiplomasia Merkel ameelekea Mazar-i-Sharif kambi kuu ya vikosi vya Ujerumani ilioko kaskazini mwa Afghanistan.