KABUL: Jemadari wa ISAF aomba msaada zaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 29.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Jemadari wa ISAF aomba msaada zaidi

Majeshi ya kimataifa yanayosaidia kulinda usalama nchini Afghanistan-ISAF yana upungufu wa vikosi na zana.Hayo,ni kwa mujibu wa mkuu wa Kijerumani wa vikosi vya ISAF.Jemadari Bruno Kasdorf alizungumza kwa simu ya video kutoka mji mkuu wa Afghanistan,Kabul pamoja na wizara ya ulinzi ya Ujerumani mjini Berlin.Amesema,kazi za kuijenga upya Afghanistan zitasaidiwa sana ikiwa wanajeshi elfu kadhaa zaidi,watapelekwa nchi hiyo.Jemadari Kasdorf akaeleza kuwa wanajeshi 40,000 waliokuwepo hivi sasa Afghanistan hawatoshi. Amesema,wanajeshi zaidi wanahitajiwa kwa sababu wanamgambo wa Taliban wanazidi kufanikiwa kuingia katika yale maeneo ambako vikosi vya ISAF huondoka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com