1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Askari wanne wameuwawa kwenye shambulio la bomu

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7G6

Takriban askari wanne wameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa katikashambulio la bomu katika mji wa Gereshk ulio kusini mwa jimbo la Helmund nchini Afghanistan.

Mlipuko huo ulitokea wakati ambapo watu walikuwa katika pilika pilika za kusherehekea sikukuu ya Idd baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Shambulio jingine limemuua mtoto mmoja na kuwajeruhi watoto wawili wakati kombora lililongwa dhidi ya jumba la serikali kukosea shabaha na kuangukia katika nyumba moja huko mashariki mwa jimbo la Kunar.