1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juventus wawinda ubingwa mara ya 6 mfululizo

18 Mei 2017

Nchini Italia huenda Juventus wakaishinda ligi kuu ya nchini humo Serie A bila hata kukanyaga uwanjani kwa mechi yake ya mwisho.

https://p.dw.com/p/2dCKV
Juventus vs. Chievo Gonzalo Higuain jubelt mit Sami Khedira
Picha: Getty Images/AFP/M. Bertorello

Wapinzani wake wakuu katika kuliwania taji hilo AS Roma na Lazio watakuwa wanacheza mechi zao siku ya Jumamosi, na iwapo watapata sare au kushindwa kwenye mechi hizo basi Juventus watakuwa wamejinyakulia ubingwa wa Italia kwa mara ya sita mfululizo. Juventus watacheza dhidi ya Crotone Jumapili.

Hilo litakuwa kombe la Juve katika kipindi cha chini ya wiki moja baada ya kuwaangusha Lazio 2-0 katika kombe la Italian Cup Jumatano. Klabu hiyo iliyo chini ya ukufunzi wa Massimiliano Allegri, bado ina nafasi ya kushinda mataji matatu msimu huu kwa kuwa wana fainali ya ligi ya vilabu bingwa dhidi ya Juventus inayowasubiri tarehe 3 Juni ambapo watakuwa wanaoneshana ubabe na Real Madrid huko Cardiff, Wales.

Roma wanaoshikilia nafasi ya pili watakuwa wanapambana na Chievo Verona ugenini kisha Napoli walio katika nafasi ya tatu wavaane na Fiorentina. Ushindi kwa Roma utaongeza shinikizo kwa Juventus kwasababu watakuwa wamepunguza tofauti ya alama iliyoko baina yao hadi alama moja, kabla hao The Old Lady hawajachuana na Crotone wanaopigania wasishushwe daraja.

Pescara na Palermo wao tayari washashushwa daraja ingawa Crotone bado wana nafasi ya kukwepa kushuka katika ligi ya daraja la pili Serie B. Ushindi mara 5 na sare 2 katika zao saba zilizopita ni jambo lililowapelekea kupunguza tofauti ya alama baina yao na Empoli wanaoshikilia nafasi ya 17 hadi kufikia alama moja pekeyake, nao Empoli wao watakuwa wana kazi ngumu ya kutafuta alama tatu kwa Atalanta ambao kwa sasa ni moto wa kuotea mbali.

Mwandishi: Jacob Safari/APE

Mhariri: Bruce Amani