1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya za haki-binadamu

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCer

LONDON:

Jumuiya za haki za binadamu ulimwenguni, zimeelezea masikitiko yake juu ya kunyongwa kwa Saddam Hussein.

Zimnesema unyongaji wake umekwenda kinyume kabisa na utawala wa sheria na hautasaidia kitu kukomesha umwagaji damu nchini Iraq.

Wakati mashirika kama Amnesty International na Human Rights Watch, yanaafikiana kuwa Saddam alistahiki kuhukumiwa, yameeleza juu ya hivyo, masikitiko makubwa kwamba amenyongwa.Chama cha Amnesty International kimesema kinapinga mtindo wa kunyonaga ulimwenguni.