Jumuiya ya kimataifa kusaidia demokrasia Belarus | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.02.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Jumuiya ya kimataifa kusaidia demokrasia Belarus

Kiasi cha euro millioni 87 kimeahidiwa kutolewa kwa ajili ya kusaidia makundi ya kijamii nchini Belarus.

default

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko

Ahadi hizo zilitolewa katika mkutano wa kuchangisha fedha kuyasaidia makundi hayo uliyomalizika jana katika mji mkuu wa Poland Warsaw na kuudhuruiwa na takriban mataifa 40.

Katika mkutano huo kwa kiasi fulani ilikuwa kama ni tamasha la ufadhili.Dakika baada ya dakika kiwango cha ahadi kilikuwa kikiongezeka, ambapo jumuiya ya kimataifa imetoa fedha hizo kusaidia kuundwa kwa demokrasia nchini Belarus.

Wenyeji Poland waliahidi kutoa kiasi cha Euro millioni 10, Kamisheni ya Umoja wa Ulaya euro millioni 15.6, Marekani Dolla millioni nne na Ujerumani ikaahidi kutoa kiasi cha euro millioni 6.6, kiasi hicho pamoja ahadi nyingine zilizotolewa zilifikia kiasi cha euro millioni 87.

Fedha hizo zitakwenda kwa makundi yanayojishughulisha na masuala ya haki za binaadamu nchi humo, vyombo huru vya habari pamoja na wanafunzi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Carl Bildt akizungumza katika mkutano huo,alsiema kikao hicho ni ishara si tu kwa Belarus, bali kwa eneo lote la Ulaya katika kile ambacho wanakitetea.

´´Ishara ambayo tunatoa hii leo kuhusiana na Belarus siyo tu ni ishara kuhusiana na Belarus, bali ni ishara pia kwa kile ambacho tunakisimamia katika eneo lote la Ulaya na majirani zake, na nimuhimu kwamba tunajishulisha nacho´´alisema

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland iliyokuwa mwenyeji wa mkutano huo,Radoslaw Sikorski,aliupongeza mshikamano uliyoonyeshwa kuwaunga mkono wanaharakati wa Belarus .

´´Tumebaini kwamba utawala wa Lukaschenko umekuwa ukisaidia baadhi ya vikundi vya upinzani.Hata hivyo ukandamizaji bado unaendelea.Baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wa upinzani wameendelea kuwekwa ndani.Tunategemea kwamba wafungwa wote wa kisiasa wataachiwa huru´´

Serikali ya Poland hapo kabla ilikuwa tayari imekwishaanza harakati za kutoa nafasi kwa wananchi wa Belarus, ambapo ilitangaza kuondoa ada ya visa kwa wanafunzi kutoka nchini humo wanaotaka kwenda Poland kusoma.Nchini Poland kuna vyuo vikuu na vingine vya elimu ya juu takriban 100 ambapo wanafunzi kutoka nchi jirani wanaomba ufadhili wa kusoma.

Patricia Flor ambaye ni kamishna anayehusika na masuala ya Ulaya Mashariki katika wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani aliahidi kwamba Ujerumani itafuata mfano huo uliooneshwa na Poland.Ahadi ya msaada wa euro millioni 6.6 ambapo serikali ya shirikisho la Ujerumani imeutoa katika mkutano huo, zitatumika kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi, mafunzo kwa ajili ya waandishi wa habari na kufadhili miradi inayohusika na masuala ya demokrasia huko Belarus.Aidha amesema siasa za Ujerumani kuelekea Belarus ni za namna mbili.

´´Hiyo ina maana kwamba Ujerumani imeweka vizuizi vya kuingia halikadhalika vizuzi vya mali dhidi ya maafisa wa Belarus.Aidha kwa upande mwengine lakini,tunayasaidia makundi ya kijamii huko Belarus.Siyo tu wananchi wa Belarus ambao hawatakiwi kutaabika lakini pia hata wale wanaowaunga mkono´´

Hata hivyo pamoja na ukosoaji wote huo dhidi ya Rais Lukaschenko, lakini Waziri wa Nje wa Poland Radoslaw Sikorski amesema kuwa Umoja wa Ulaya umeweka mlango wazi wa kuingia katika mazungumzo na utawala huo, lakini kwa masharti kwamba sera za ukandamizaji zinamalizwa.

Mwandishi:Ludger Kazmierczak/Aboubakary Liongo

Mhariri:Thelma Mwadzaya

http://daletweb.dwelle.de/basebrowser/titles_details.php?title_id=10660451

Ende

►Teaser:

 • Tarehe 03.02.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/109jX
 • Tarehe 03.02.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/109jX

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com