1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jumuiya nne za kiislamu za unda Baraza Ujerumani

12 Aprili 2007

Jumuiya 4 za kiislamu zimeunda Baraza litakalotumika kama msemaji wa waislamu humu nchini .Serikali ya Ujerumani imelikaribisha lakini kuna wale wanaolikosoa.

https://p.dw.com/p/CHGQ

Jumuiya 4 za kiislamu zimeungana chini ya paa moja nchi Ujerumani na hatua yao hiyo inatafsiriwa kurahisisha mazungumzo na mawasiliano kati ya waislamu na serikali ya Ujerumani katika maswali yanayowahusu waislamu humu nchini.

Waziri wa ndani wa Ujerumani Bw. Schauble ameikaribisha hatua hii .Uchambuzi wa Gudula Geuther mnasimuliwa sasa studioni na Ramadhan

Wakati waziri wa ndani Schauble ameikaribisha mikono 2 hatua hiyo, kuna wanaoikosoa wakielezea hofu na wasi wasi kuwa Baraza hilo jipya la waislamu likigeuka mshirika m kubwa katika meza ya mazungumzo na serikali,litafanya hivyo bila ya ridhaa ya waislamu wengi nchini humu.

Katika Baraza hilo jipya la waislamu linajumuisha Jumuiya ya Milli Görus ambayo kitambo sasa inakodolewa macho na Idara ya usalama ya Ujerumani.Kwa jumla, jumuiya hizo 4 zinaangaliwa kuwa ni za kihafidhina.

Mjumbe wa chama-tawala cha SPD anaehusika na maswali ya waislamu Lale AKgün ameelöezea wasi wasi ikiwa Baraza hili litapewa mamlaka ya kutafsiri nini uislamu humu nchini.Kwani, likachiwa mamlaka hayo,hakutakua na uhuru tena kwa nadhari za kiliberali.

Kile ambacho jumuiya hizo 4 zimefanya si zaidi ya jaribio kutimiza mahitaji ya wanasiasa humu nchini bila kujali shaka shaka na hatari zake.Huu ni mwanzo unatoa nafasi zote.Masilahi ya wanasiasa yapo wazi.

Wanapohitaji sikio la kuwashauri juu ya maswali ya kiislamu, mfano wa mafunzo ya dini katika shule za serikali,kutoa nasaha kwa wafungwa gerezani,mazungumzo juu ya maadili ya kijamii, wanajua sasa wawasilane na nani.Hata waislamu nao waishio humu nchini wana chombo sasa cha kuwasiliana na serikali.Hii ni njia ya maana na barabara lakini, wakati huo huo yaonesha hatari ya mradi huu mzima….
Nani Jumuiya hizo kubwa zinawakilisha ni vigumu kusema.Kwani idadi tu haielezi ukweli.Kwa idadi tu ya wanachama au wafuasi,si dhahiri-shahiri iwsapo mkuu wa ukoo anajiwakilisha binafsi au ukoo wake mzima na kwa jumuiya zisizowakilishwa ndani ya baraza hili ni sawa tu….

Na pale penye nadharia za kizamani- mfano juu ya nafasi ya wanawake katika jamii na iwapo watoto wao wakike washiriki katika mafunzo ya kuogolea mashuleni au la, au wavae hijabu mashuleni au la,ni vigumu kuafikiana sawa na ilivyo na jumuiya nyengine nje ya Baraza hili.Jumuiya ya ALEWIT hata haikualikwa kujiunga na Baraza hilo la waislamu na hivyo, haikuonesha hamu yoyote kushirikiana nalo.

Hizo zote ni shida ambazo wanasiasa wanabidi kuzizingatia katika kiu chao cha kujipatia msemaji wa waislamu .Dhidi ya Baraza hilo, ni kuweka matarajio ya kupindukia.Na hakuna sababu za kuweka matumaini kama hayo.Bado si wazi, Baraza hilo litachangia nini na lina uwezo gani.Wakati utaonesha .

Hakuna cha kupinga kuwa na mazungumzo siku zijazo na waislamu nchini Ujerumani katika safu mbali mbali.Katika meza ya duara ambayo imeonesha mafanikio huko Bavaria na Baden Würtemberg katika kupanga nini kimwemo katika mafunzo mashuleni…

Mchango wa Baraza hili jipya lililoasisiwa ni kuwapa wanachama wake fursa ya kujumuika pamoja na kuafikiana yale wanayopigania.Hii inahitaji kwanza, pawepo utayarifu wa kuvumiliana na jambo hilo pekee nila kuthaminiwa.