1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuufumbua mzozo wa Guinee

Oummilkheir13 Februari 2007

Sheria ya hali ya hatari yapuuzwa nchini Guinee

https://p.dw.com/p/CHKI
Maaandamano nchini Guinee
Maaandamano nchini GuineePicha: picture-alliance / dpa

Wakaazi wa Guinee wamefungiwa majumbani mwao hii leo ambapo sheria ya kutotoka nje imeanza kufanya kazi katika nchi hiyo ya Afrika magharibi.Hata hivyo risasi zinafyetuliwa na vijana wamepania kuteremka majiani kuandamana,licha ya dazeni kuuwawa katika machafuko ya hivi karibuni.

Rais Lansana Konte ametangaza sheria ya hali ya hatari jana usiku.Uamuzi huo umefuatia siku tatu za machafuko kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji ambapo watu wasiopungua 27 wamepoteza maisha yao,baada ya wakuu wa vyama vya upinzani na vyama vya wafanyakazi kuitisha mgomo kumtaka rais Konte ajiuzulu, waakilalamika dhidi ya kuendewa kinyume makubaliano ya kugawana madaraka.

“Mizinga baado inafyetuliwa,hakulaliki kwasababu ya milio ya risasi.” Amesema Aissatou Diallo,ambae ni mkaazi wa Madina,.karibu na mji mkuu Conakry.

“Toka roshanini kwangu nawaona watu wametoka nje,wanakwenda kuuza na kunua vitu sokoni.Hata baadhi ya taxi ziko njiani” Ameendelea kusema bibi huyo.

Kwa upande wake Jean Claude Diallo,mshauri wa serikali ya mji mjini Frankfurt,ambae aliwahi wakati mmoja kua waziri katika serikali ya rais Lansana Konte nchini Guinee anasema:

“Namuomba Mungu aisadie Guinee,kwa sabababu hali namna ilivyo inatisha.Pekee busara ndiyo itakayotunusuru na kututoa katika balaa.”

Ubalozi wa Marekani umewaamuru watumishi wake wote waihame Guinee.Hata raia wa kawaida wa Marekani wametakiwa waaihame nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Ndege maalum ya serikali ya Marekani imetolewa kuwasafirisha watumishi wa ubalozi na raia wa Marekani hadi Dakar mji mkuu wa Senegal.

Mzozo wa Guinee umewatia mbioni pia viongozi wa nchi jirani.Rais Ahmad Tejan Kabbah wa Sierra Leone amesema viongozi wan chi za Afrika magharibi watakutana haraka kusaka ufumbuzi wa mzozo huo.

“Nimezungumza binafsi na rais Lansana Conte na maafisa wengine wa serikali wanaohusika na mzozo” amesema rais Kabbah ambae nchi yake ndio kwanza imeanza kuchipuka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika miaka mitano iliyopita.

Rais Ahmad Tejah Kabbah amesema kupitia Radio ya taifa,amemuarifu naibu waziri mkuu wa Uengereza John Prescott kwamba mataifa 15 ya jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi ya afrika Magharibi-ECOWAS na Umoja wa nchi zinazopakana na Mto Mano,wameingia mbioni kuufumbua haraka mzozo wa Guinee .

“Hali inatutia wasi wasi sote viongozi wa eneo hili! Ameshadidia rais Kabbah.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Sierra Leone-APC,Ernest Koroma amewatolea mwito viongozi wa mataifa yenye nguvu katika eneo hilo “yaingilie kati haraka ili kuepusha balaa la matumizi ya nguvu.”

“Matukio ya Guinee,naiwe kisiasa,kiuchumi au kibiashara yanashawishi haraka hali ya mambo nchini Sierra Leone-inamaanisha Guine wakewnda chafya,basi na walioko Sierra wanashikwa na mafua.”Mwisho wa kumnukuu Ernest Koroma wa chama cha Upinzani cha Sierra Leone-All People Congress.