1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JUBA:Ban Ki Moon awasili Juba

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewasili katika mji wa kusini mwa Sudan wa Juba kujaribu kumiraisha mpango wa amani wa mwaka 2005 uliyohitimisha vita vya miongo miwili vya wenyewe kwa wenyewe.Mpango huo kwa sasa uko katika hatari ya kuvunjika.

Ban Ki Moon anategemewa kukutana na kiongozi muasi wa zamani ambaye ni sasa ni Makamu wa kwanza wa Rais Salva Kirr ambaye alichukua uaongozi wa kundi la SPLM kufuatia kifo cha John Garang mwaka 2005.

Umoja wa wa Matifa una kikosi cha askari 10,000 katika eneo hilo la Juba kinachohakikisha mkataba wa amani unatekelezwa.

Hata hivyo ziara hiyo ya Ban Kin Moon ni mahsusi kwa ajili ya kuharakisha kufikiwa kwa mpango wa amani katika jimbo lenye mzozo la magharibi mwa Sudan la Darfur.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja pia alisema kuwa Rais Omar Hassan Al Bashir ameamuahidi kuwa mkuu wa waasi wa Darfur Sulaiman Jamous ataruhusiwa kusafiri nje ya nchi kwenda kupata matibabu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com