1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOLO:Wanajeshi 9 wauwawa na wanamgambo wakiislamu ufilipino

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaq

Wanajeshi wa ufilipino wamearifu kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wakiislamu wamewauwa wanajeshi tisa wa serikali katika uvamizi uliofanywa huko kusini mwa kisiwa cha Jolo.

Inasemekana wanajeshi wawili pia walijeruhiwa kwenye shambulio hilo lililotokea karibu na mji wa Maimbung.

Wanajeshi wa serikali wamekuwa wakiendesha opresheni dhidi ya waasi wa Abu Sayyaf wanaohusishwa na kundi la mtandao wa kigaidi la alqaeda walioko katika kisiwa cha Jolo tangu mwaka jana.