1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

John Atta Mills rais mpya wa Ghana

Jane Nyingi7 Januari 2009

Ghana ina rais mpya John Atta Mills. Atta mills kutoka chama cha upinzani, aliapishwa katika sherehe iliyoandaliwa, uwanja wa Uhuru mjini Accra.

https://p.dw.com/p/GTqY
Rais wa Ghana John Atta MillsPicha: AP

Maelfu ya Waghana walijiunga na marais kadhaa kutoka mataifa ya magharibi mwa bara la afrika kushuhudia halfa hiyo.

Huu ni mkusanyiko mkubwa wa watu kuwahi kuhudiwa nchini humo kwa zaidi ya miaka 10. Atta Mills Kutoka chama cha upinzani alimshinda kwa kura chache mpinzani wake kutoka chama tawala kufuatia marudio ya uchanguzi mkuu yaliyofanyika jumamosi iliyopita.

Rais John Kufour anaondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa kipindi kinachokubalika kisheria cha mihula miwili. Atta Mills ambaye awali alikuwa amegombea urais mara mbili dhidi ya Kufour na kushindwa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuumarisha uchumi wa Ghana na kuwaunganisha waghana ambao tayari walikuwa wamegawanyika kisiasa kutokana na uchaguzi huo mkuu

Ndugu na dada zangu wacha niseme uchaguzi umekwisha, kwasasa tuna Ghana moja, hakuna NDC Ghana, hakuna NPP Ghana hakuna CCP Ghana kuna Ghana moja„

Ghana ni mojawapo ya mataifa machache katika bara la afrika kubadilishana mamlaka ya urais mara mbili kupitia rais aliyechanguliwa kihalali. Wachanganuzi wanasema hatua hiyo ni dhihirisho tosha kuwa Ghana imekomaa kidemocrasia baada ya enzi za mapinduzi na uditeta katika miaka ya 70 na 80.

Kulikuwepo na hali ya wasiwasi wakati wa uchaguzi mkuu na mgombea urais kwa chama tawala nchini Ghana Nana Akufo Addo alikuwa ametishia kuyakataa matokeo ya uchaguzi huo. Hata hivyo aliondoa malalamishi aliyokuwa ameyawasilisha mahakamani na kukubali kushindwa kwa njia ya amani.

Umoja wa afrika umepongeza uchanguzi huo mkuu ambao mgombea wa chama cha upinzani John Atta Mills aliibuka mshindi na kusema ni ishara ya matumaini kwa bara la afrika.

Mapema hivi leo bunge jipya nchini Ghana lilingia ofisini na kumchagua mwanamke kuwa spika. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kumchagua mwanamke kuwa spika tangu lilipopata uhuru mwaka 1957. Sherehe za kuapishwa kwa Atta millis mwenye umri wa miaka 64 zilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Afrika akiwemo Laurent Gbagbo wa IvoryCoast, Bi.Ellen Sirleaf wa Liberia , Blaise Compaore wa Burkinafaso na rais Abdoulaye Wade wa Senegal.


►◄