1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG:Wauguzi na walimu waandamana

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvt

Mashirika ya wafanyikazi yanayowakilisha wafanyikazi milioni moja wa sekta ya umma wameandamana hii leo ili kudai nyongeza ya asilimia 12 ya mshahara.Maandamano hayo yameathiri shughuli katika shule na hospitali nchini humo.Serikali kwa upande wake imeahidi nyongeza ya asilimia 6 kwa kuhofia athari za kiuchumi unaokabiliwa na mfumko wa bei uliopita asilimia 6 kwa sasa.Hii ni mara ya kwanza umefikia viwango hivyo katika kipindi cha miaka mine.

Mazungumzo ya kufikia muafaka yalivunjika mapema wiki hii.Kulingana na vyama vya wafanyikazi mishahara yao ni ya chini sana jambo linalopelekea kuondoka kwa wingi kwa wauguzi na waalimu kutafuta kazi katika mataifa mengine.

Kinachowaudhi zaidi ni nyongeza ya asilimia 50 ya mshahara wa wanasiasa wa ngazi za juu .Waandamanaji hao walikusanyika katika miji mikuu ili kuwasilisha malalamiko yao.