1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG : Merkel akutana na Mandela

6 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hz

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekutana na rais mstaafu wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela leo hii mjini Johannesburg.

Merkel ameuelezea mkutano wake wa dakika 45 na Mandela kuwa umemgusa sana na kwamba wamejadili haja ya kutatuwa mizozo ya Afrika kwa amani.Merkel amesema ujumbe wa Mandela ni kwamba wanahitaji amani duniani hususan mizozo barani Afrika lazima itatuliwe kwa njia ya amani.Pia wamegusia tatizo la UKIMWI ambalo limekuwa hasa likiiathiri Afrika Kusini ambapo watu milioni 5.5 wa idadi ya watu milioni 48 nchini humo wanaishi na virusi vya HIV.

Kansela Merkel pia ameitumia ziara yake nchini Afrika Kusini kumhimitza Rais Thabo Mbeki wa nchi hiyo kuchukuwa hatua kali zaidi kumshawishi Rais Robert Mugabe kukomesha ukiukaji wa haki za binaadamu.

Rais Mbeki msuluhishi wa mzozo wa Zimbabwe kati ya serikali na wapinzani anasema tuna imani kabisa kutakuwepo na matokeo mazuri ambayo yatapelekea kuwepo kwa hali ya kisiasa ambayo itashughulikia mgogoro huu mbaya kabisa wa kiuchumi.

Ziara ya Merkel barani Afrika pia imemfikisha Ethiopia na ataikamilisha hapo kesho kwa kutembelea Liberia.