1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Laila Ali amshinda Gwendolyn O'Neal kwa knock-out.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV4

Laila Ali, binti yake Mohamed Ali bondia wa zamani bingwa wa uzani wa juu duniani, amemrambisha sakafu Gwendolyn O´Neil wa Guyana jana katika dakika ya hamsini na sita ya raundi ya kwanza ya pambano lao kuwania mkanda wa Baraza la Ndondi duniani katika uzani wa Super-Middle.

Laila amewataka radhi mashabiki waliokuwa wamehudhuria pambano hilo mjini Johannesburg, Afrika Kusini, kwani alimaliza kazi mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela, alikuwa miongoni mwa mashabiki waliomshuhudia Laila akifanya mambo yake jukwaani.

Laila Ali mwenye umri wa miaka ishirini na tisa sasa ana rekodi ya kushinda mapigano ishirini na manne tangu alipojitosa kwenye ulingo wa ndondi za kulipwa mwaka elfu moja mia tisa na tisini na tisa.

Miongoni mwa mapigano yote hayo, Laila Ali ameshinda mapigano ishirini na moja kwa njia ya knock-out.