1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JINJA:Kikosi cha kulinda amani cha Uganda chaanza safari

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNT

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anatangaza kuwa majeshi ya nchi yake ya kulinda amani nchini Somalia hayana lengo la kuwasalimisha wapiganaji nchini humo.Majeshi hayo ya Uganda ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika kilichoidhinidhwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu umeshambuliwa na wanamgambo tangu jeshi la Somalia lilikishirikiana na jeshi la nchi jirani ya Ethiopia lilipowafurusha wapiganaji wa mahakama za kiislamu mwezi Disemba mwaka jana.

Takriban maafisa 30 wa kijeshi waliwatangulia majeshi yao mjini Baidoa kama sehemu ya kwanza ya kikosi cha majeshi alfu 8 cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani.

Kulingana na msemaji wa jeshi wa kikosi cha Somalia Paddy Ankunda kikosi cha vifaru kinatarajiwa kusafiri kutoka mombasa nchini Kenya kwa reli kisha kwa meli hadi mji wa Mogadishu.Mkuu wa jeshi Arunda Nyakairima anaonya majeshi hayo kuchukua tahadhari katika operesheni nzima.

Mpaka sasa Umoja wa Afrika AU umepata nusu ya majeshi yote yanayohitajika ambayo ni alfu 8.Nchi ya Burundi imeahidi kuchangia majeshi 1700 vilevile Nigeria iliyoahidi wanajeshi 850.Nchi nyingine zilizotoa ahadi hiyo ni Malawi na Ghana.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi anapanga kuondoa majeshi yake nchini Somalia haraka iwezekanavyo baada ya kuonya kuwa nchi yake huenda ikawa na hatari ya kuvamiwa na wapiganaji wa kiislamu.