JIDDAH : Wanausalama wapambana na magaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JIDDAH : Wanausalama wapambana na magaidi

Vikosi vya usalama vya Saudi Arabia hapo jana vimepambana na magaidi ambao waliwapiga risasi na kuwauwa walinzi wawili nje ya gereza ambapo watuhumiwa wa Al Qaeda wanashikiliwa katika mji wa magharibi mwa nchi hiyo wa Jiddah.

Kituo cha televisheni cha Al Jazeera chenye makao yake huko Qatar kimeripoti kwamba wanamgambo wawili walitiwa mbaroni lakini jambo hilo halikuweza kuthibitishwa mara moja. Polisi ilikuwa imelizingira jengo ambako watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wamejificha kwenye eneo karibu na gereza la Ruwais.

Mashahidi wanasema helikopta zilikuwa zikilizunguka eneo hilo na magari ya deraya yalilizingira jengo hilo lilikouwa limemurikwa na mwanga mkubwa wa mataa.

Mapigano hayo yalianza pale watu hao wenye silaha walipowafyatulia risasi walinzi walioko nje ya gereza na kuuwa wawili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com